851 Madereva Jobs at United Republic Of Tanzania - Career Opportunity in Tanzania
Website :
1878 Days Ago
Linkedid Twitter Share on facebook

Vacancy title:
851 Madereva

 

Jobs at:
United Republic Of Tanzania

Deadline of this Job:
3rd April 2019  

Duty Station:
Dar es Salaam , Tanzania , East Africa , 00000 , TZ

Summary
Date Posted: 22nd March 2019 , Base Salary: Not Disclosed , Employment Type: Full_Time , Currency: TZS , Value: 625000 , Minimum: 437500 , Maximum: 1875000 , Period: MONTH

 

JOB DETAILS:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/J/17 21 Machi, 2019
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali anakaribisha maombi ya kazi ya Madereva watakaoajiriwa katika Ofisi tofauti Serikalini kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi za kazi 851 kama inavyooneshwa katika tangazo hili.
851 Dereva Daraja La II TGS B.

MAJUKUMU YA KAZI
• Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
• Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
• Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
• Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
• Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,
• Kufanya usafi wa gari, na
• Kufanya kazi nyingine kadri anavyoelekeza na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa kwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya Daraja la E au C1 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka bila kusababisha ajali.
• Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
• Waombaji wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.

 

{module 312}

Job application procedure
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
• Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
• Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
• Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
• Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
• Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
• Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
• Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
• Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
• Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
• Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 03 Aprili, 2019.
• Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
• Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/  (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA KAZI
ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU. ANUANI YA BARUA HIYO
IELEKEZWE KWA
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P 63100 DAR ES SALAAM.

 

Job Info
Job Category: Transportation jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 3rd April 2019
Duty Station: Dar es Salaam , Tanzania
Posted: 22-03-2019
No of Jobs: 851
Start Publishing: 22-03-2019
Stop Publishing (Put date of 2030): 22-03-2065
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.