Vacancy title:
Contract Teacher Positions in Secondary Schools for Business Studies Subject-Arusha
[Type: VOLUNTEER, Industry: Public Administration, and Government, Category: Education, Civil & Government, Teachers & Education]
Jobs at:
Prime Minister’s Office
Deadline of this Job:
Sunday, June 14 2026
Duty Station:
Arusha | Arusha
Summary
Date Posted: Tuesday, June 2 2026, Base Salary: Not Disclosed
Similar Jobs in Tanzania
Learn more about Prime Minister’s Office
Prime Minister’s Office jobs in Tanzania
JOB DETAILS:
Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa kushiriakiana na asasi ya Educate! Tanzania kupitia mradi wa kuboresha Ufundishaji na Ujifunzaji wa Somo la Elimu ya Biashara (Business Studies), inatekeleza afua ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Elimu ya Biashara (Business Studies). Ofisi inatangaza nafasi 400 za walimu wa kujitolea (mkataba) wa somo la Elimu ya Biashara kwa ajili ya shule za Sekondari zenye uhitaji mkubwa, kwenye mikoa ifuatayo: Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Simiyu, Kagera, Geita, Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani, na Dar es Salaam. Lengo la mradi huu ni kufanikisha utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023 na Mtaala ulioboreshwa wa Elimu ya Sekondari unaoelekeza ufundishwaji wa Somo la Elimu ya Biashara ili kuongeza ujuzi wa ujasiriamali kwa wanafunzi. Hivyo, wahitimu wa Shahada (Degree) kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kujitolea kufundisha Somo la Biashara katika shule za sekondari zitakazoorodheshwa kupitia Mfumo Rasmi wa Maombi ya ajira kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI. Muda wa kuwasilisha maombi ni kuanzia tarehe Juni hadi 14 Juni, 2026. Walimu wa Kujitolea (mkataba) watakaokidhi vigezo watapangwa na kusimamiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
1.0 TARATIBU ZA KUOMBA
Waombaji wenye sifa wawasilishe maombi kupitia kiunganishi ajira.tamisemi.go.tz.
Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Shahada ya Ualimu katika masomo ya Biashara na Shahada ya Fani za Elimu ya Biashara au Uchumi (Degree in Business related fields or Economics) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
2.0 SIFA ZA KITAALUMA ZA MWOMBAJI
Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
1. Shahada (Degree) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali katika moja ya
fani hizi:
○ Shahada ya Ualimu katika Masomo ya Biashara - (Bachelor of Education in Business Studies / Business Education)
○ Shahada ya Biashara - (Bachelor of Commerce – BCom)
○ Shahada ya Usimamizi wa Biashara - (Bachelor of Business Administration– BBA)
○ Shahada ya Uchumi au Shahada ya Sanaa katika Uchumi - (Bachelor of Economics / Bachelor of Arts in Economics)
○ Shahada katika Fani Nyingine Zinazohusiana na Masomo ya Biashara - (Bachelor’s Degree in Other Business-Related Fields)
2. Taaluma ya msingi ya biashara, hata kama hana uzoefu wa kufundisha.
3. Uwezo wa kutumia kompyuta kwa shughuli za msingi za ufundishaji na ujifunzaji.
3.0 MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI
(i) Awe raia wa Tanzania;
(ii) Awe na umri usiozidi miaka 42;
(iii) Aambatishe nakala ya cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha Nne na au Kidato cha Sita, na Fani ya Taaluma aliyosomea.
(iv) Awe tayari kufanya kazi katika Shule za Sekondari zenye mahitaji makubwa ya walimu.
(v) Mwombaji atakayechaguliwa hataruhusiwa kubadilisha kituo au shule atakayopangiwa awali katika kipindi cha utekelezaji wa programu hii ya kujitolea.
(vi) Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine;
(vii) Awe hajawahi kufukuzwa au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma kwa makosa ya kiutumishi;
(viii) Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA);
(ix) Waombaji waambatishe nyaraka zote muhimu katika mfumo;
(x) Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwa kupata
Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi
EQ… kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na waliosoma vyuo vya nje; na
(xi) Aambatishe barua ya maombi
Work Hours: 8
Experience in Months: 24
Level of Education: bachelor degree
Job application procedure
For additional information regarding applicant qualifications and application procedures, please contact the Prime Minister's Office – TAMISEMI customer service center by phone at 026 2160210 or 0735 160210 from 8:00 AM to 8:00 PM on working days.
The deadline for receiving applications is June 14, 2026, at 11:59 PM.
Application Link:Click Here to Apply Now
Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.