Materials Technician job at The Tanzania National Roads Agency (TANROADS)sss
Website :
460 Days Ago
Linkedid Twitter Share on facebook
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Makatibu Wakuu wa Wizara, Watendaji Wakuu wa Idara zinazojitegemea, Watendaji wakuu wa Mamlaka/Wakala za Serikali, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji/Manispaa/Miji na Wilaya anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi Mia Tatu Sabini na Mbili (372) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.


1.0.0 MHANDISI UMEME - MITAMBO (ELECTRO-MECHANICAL) DARAJA LA II – NAFASI 4

1.1.0 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu Umeme na mitambo mbalimbali, bei za mitambo na vifaa vya umeme ndani na nje ya nchi;
ii. Kuhakikisha uthamani sahihi wa kazi ili kufikia thamani ya fedha;
iii. Kupanga, Kubuni na Kutengeneza Mitambo chini ya Mhandisi aliyesajiliwa
(Professional Engineer) iv. Kufanya Usanifu na kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Ufundi na Umeme
(Electrical and Mechanical Projects);
v. Kufanya Ukaguzi na matengenezo ya kawaida na matengenezo kinga ya vifaa vya kazi, Ufundi na mitambo;
vi. Kusanifu, kuandaa gharama na kufanya matengenezo ya miradi ya Umeme na
Ufundi (Electrical and Mechanical Projects); vii. Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu vifaa vya umeme na mitambo mbalimbali ndani na nje ya nchi;
viii. Kuandaa na kutunza kanzidata ya mitambo pamoja na matengenezo yake; na
ix. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
1.2.0 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyefuzu mafunzo ya Shahada ya kwanza ya Uhandisi katika fani ya Umeme na Mitambo (Electro-Mechanical) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta na waliosajiliwa na Bodi ya Wahandisi kama Graduate Engineer (GE).
1.3.0 NGAZI YA MSHAHARA - Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS
E1

1.4.0 MHANDISI UMEME (ELECTRICAL – POWER (RENEWABLE ENERGY) DARAJA LA II – NAFASI 1

1.5.0 KAZI NA MAJUKUMU

i. Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu Nishati ya Umeme pamoja na bei za vifaa vya umeme ndani na nje ya nchi;
ii. Kuhakikisha uthamani sahihi wa kazi ili kufikia thamani ya fedha;
iii. Kupanga, Kubuni na Kutengeneza Mitambo chini ya Mhandisi aliyesajiliwa
(Professional Engineer); iv. Kufanya Usanifu na kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Ufundi na Umeme
(Electrical and Mechanical Projects);
v. Kufanya Ukaguzi na matengenezo ya kawaida na matengenezo kinga ya vifaa vya kazi, Ufundi na Umeme;
vi. Kusanifu, kuandaa gharama na kufanya matengenezo ya miradi ya Nishati ya
Umeme na Ufundi (Electrical and Mechanical Projects); vii. Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu vifaa vya umeme na mitambo mbalimbali ndani na nje ya nchi; na
viii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
1.6.0 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyefuzu mafunzo ya Shahada ya kwanza ya Uhandisi katika fani ya Umeme wa Umeme (Electrical-Power) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta na waliosajiliwa na Bodi ya Wahandisi kama Graduate Engineer (GE).
1.7.0 NGAZI YA MSHAHARA - Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali –
TGS E1

1.8.0 MHAIDROLOJIA DARAJA LA II – (HYDROLOGIST II) NAFASI 16

1.9.0 KAZI NA MAJUKUMU YA MHAIDROLOJIA DARAJA LA II

i. Kusimamia ujenzi na ukarabati wa vituo vya hali ya hewa na vituo vya upimaji wa wingi wa maji kwenye mito, mabwawa na maziwa;
ii. Kufanya uhakiki wa takwimu (validation activities) wakati wa kuchakata takwimu;
iii. Kuandaa mipango na michoro mingine ya mtandao wa uchunguzi (observation networks) wa kihaidrolojia na kimetorolojia;
iv. Kuandaa mipango, kusanifu, kusimamia shughuli za ujenzi katika vituo vya uchunguzi (observation networks);
v. Kusimamia uchunguzi wa kihaidrolojia wa uhusiano kati ya kina cha maji na wingi wa maji (stage - discharge observations);
vi. Kutengeneza ramani za vidaka maji katika mabonde ya Maji kwa kutumia njia ya
Geographical Information System (GIS); vii. Kuandaa ramani zinazoonyesha maeneo yanayoathiriwa na mafuriko katika mabonde na kushiriki katika kutoa ushauri juu ya tahadhari;
viii. Kuhakiki ubora wa takwimu zote za kihaidrolojia na kimeteorolojia;
ix. Kuratibu na kufanya uchunguzi wa awali wa shughuli zinazohusu vituo vya kihaidrolojia; na
x. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

1.10.0 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyefuzu mafunzo ya Shahada ya kwanza ya Haidrolojia au Uhandisi wa Rasilimali maji kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
1.11.0 NGAZI YA MSHAHARA - Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS E1

1.12.0 MHAIDROJIOLOJIA DARAJA II (HYDROGEOLOGIST II) – NAFASI 11

1.13.0 KAZI NA MAJUKUMU YA MHAIDROLOJIA DARAJA LA II
i. Kufanya na kusimamia utafiti wa maji chini ya ardhi wenye lengo la kubaini kiasi na ubora wa maji yaliyoko chini ya ardhi;
ii. Kufanya kazi za kihaidrojiolojia zinazohusiana na usalama wa mabwawa;
iii. Kukagua mitambo na vifaa vya makampuni yanayohitaji leseni za utafiti wa maji chini ya ardhi;
iv. Kukusanya, kuchambua na kuchakata takwimu na taarifa mbalimbali za kihaidrojiolojia kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ya Sekta ya Maji;
v. Kufanya matengenezo madogo ya vifaa vya utafiti wa maji chini ya ardhi;
vi. Kukusanya, kuchambua na kuchakata takwimu na taarifa mbalimbali za kihaidrojiolojia kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ya Sekta ya Maji;
vii. Kuratibu na kusimamia utafiti wa maji chini ya ardhi na kutoa ushauri unaohitajika na wataalam wa kada na fani zingine za Sekta ya Maji;
viii. Kuratibu na kusimamia uchimbaji wa visima na kuhakiki taarifa za kukamilika kwa uchimbaji;
ix. Kufanya usanifu wa ujenzi wa kisima (Design of well development); na
x. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

1.14.0 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyefuzu mafunzo ya Shahada ya kwanza ya Haidrojiolojia, Jiolojia, Uhandisi Jiolojia au Jiofizikia kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
1.15.0 NGAZI YA MSHAHARA - Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS E1


2.0.1 AFISA UGAVI DARAJA LA II (SUPPLIES OFFICER II) - NAFASI 15 2.0.2 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutayarisha makisio ya vifaa vinavyohitajika (Schedule of Requirements); ii. Kuandaa utaratibu wa upokeaji wa vifaa; iii. Kuandaa na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa; iv. Kusimamia upokeaji, usambazaji na utunzaji wa vifaa (Phisical Distribution);
v. Kubuni mfumo wa uwekaji na utunzaji wa vifaa ghalani (Location Index Design); vi. Kuandaa taarifa mbali mbali za vifaa;
vii. Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyomo ghalani kwa kufuata taratibu zilizopo;
viii. Kuandaa hati za kupokea vifaa
ix. Kutoa vifaa kwa watumiaji (Distribute goods to user Department and other users; na
xi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

2.0.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza/Stashahada ya Juu ya Ununuzi au Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali au wenye "Professional level Ill" inayotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (Procurement and Supplies Professionals and Technicians Board - (PSPTB); au sifa nyingine inayotambuliwa na
PSPTB na awe aliyesajiliwa na PSPTB kama "Graduate Procurement and Supplies Professional".
2.0.4 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS. D

2.0.5 AFISA UNUNUZI DARAJA LA II (PROCUREMENT OFFICER II) - NAFASI 15 2.0.6 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kushiriki katika kuandaa nyaraka za zabuni; ii. Kusambazi hati/nyaraka za zabuni;
iii. Kuwasiliana na idara mbalimbali kuhusu mahitaji ya ununuzi;
iv. Kukusanya na kutunza taarifa ya bei za soko “Market Intelligence” kwa baadhi ya bidhaa;
v. Kuhakiki hati zote za madai kabla ya malipo; vi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

2.0.7 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza/Stashahada ya Juu ya Ununuzi au Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali au wenye "Professional level Ill" inayotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (Procurement and Supplies Professionals and Technicians Board - (PSPTB); au sifa nyingine inayotambuliwa na
PSPTB na awe aliyesajiliwa na PSPTB kama "Graduate Procurement and Supplies Professional".

2.0.8 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS. D

2.0.9 AFISA UGAVI MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT SUPPLIES OFFICER II) – NAFASI 10

2.0.10 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutunza ghala la vifaa lenye thamani nyingi; ii. Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa na wazabuni mbalimbali na kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa; iii. Kufungua na kutunza “Bin Card” kwa kila kilichopo ghalani;
iv. Kufungua ledger ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vilivyoingia, kutunzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali;
v. Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine; vi. Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na kwa usalama; vii. Kuandaa hati za kupokelea vifaa; na
ix. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.



2.0.11 SIFA ZA MWOMBAJI KAZI
Stashahada ya Ugavi/Ununuzi au Biashara iliyojiimarisha kweye Ununuzi na Ugavi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali au sifa inalingana na hiyo inayotambuliwa na
Bodi ya Wataalamu wa Ugavi na Ununuzi nchini. Awe amesajiliwa na PSPTB kama
“Procurement and Supplies Technician” au “Procurement and Supplies Full Technician” na awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

2.0.12 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS. C

2.0.13 AFISA UNUNUZI MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT PROCUREMENT OFFICER II) – NAFASI 10

2.0.14 MAJUKUMU YA KAZI


i. Kutunza ghala la vifaa lenye thamani nyingi; ii. Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa na wazabuni mbalimbali na kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa; iii. Kufungua na kutunza “Bin Card” kwa kila kilichopo ghalani;
iv. Kufungua ledger ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vilivyoingia, kutunzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali;
v. Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine; vi. Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na kwa usalama; vii. Kuandaa hati za kupokelea vifaa; na viii. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.

2.0.15 SIFA ZA MWOMBAJI KAZI
Stashahada ya Ugavi/Ununuzi au Biashara iliyojiimarisha kweye Ununuzi na Ugavi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali au sifa inalingana na hiyo inayotambuliwa na
Bodi ya Wataalamu wa Ugavi na Ununuzi nchini. Awe amesajiliwa na PSPTB kama
“Procurement and Supplies Technician” au “Procurement and Supplies Full Technician” na awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

2.0.16 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS. C



2.0.17 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (OFFICE MANAGEMENT SECRETARY II) - NAFASI 15 2.0.18 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri ii. Kupokeawageni na kuwasili shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa; iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi zingine; iv Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi; v. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
vi.Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali; vii Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi na vi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

2.0.19 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye kuhitimu kidato cha nne (IV) au sita (VI) mwenye Stashahada ya uhazili (diploma) au NTA Level 6. Awe amefaulu somo la hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza, maneno 80 kwa dakika moja.

2.0.20 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS. C


2.0.21 MHANDISI- MAGARI DARAJA LA II -( AUTOMOBILE ENGINEER II) NAFASI 2

2.0.22 MAJUKUMU YA KAZI
i.Kufanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya wahandisi kama
“Professional Engineer” ili kupata uzoefu unaotakiwa.

ii.Kufanya kazi kwa vitendo katika fani zinazomhusu ili kumwezesha Mhandisi kupata sifa za kutosha kusajiriwa na Bodi ya usajili wa Wahandisi.

iii.Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu magari na Mitambo mbalimbali, bei za magari, mitambo, na vifaa vya umeme, ndani na Nje ya Nchi.

iv.Kupitia mapendekezo ya miradi (Project proposals) mbalimbali ya Ufundi yanayowasilishwa Wizarani.

2.0.23 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada/Stashahada ya juu ya Uhandisi wa Magari (Automobile Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika moja wapo ya fani za uhandisi tajwa hapo juu.

2.0.24 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS. E


2.0.25 MUUGUZI DARAJA LA II (NURSE II) – 15 POSTS 2.0.26 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitali na sehemu zote zinapotolewa huduma za afya; ii. Kusimamia na kuratibu kazi zote za wahudumu wa afya katika sehemu yake ya kazi; iii. Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji wake wa kazi; iv. Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani; v. Kutoa ushauri nasaha; vi. Kutoa huduma za kinga na uzazi wa mpango; vii. Kutoa huduma za uzazi na afya ya mtoto; viii. Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya; ix. Kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi; na x. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
2.0.27 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.
2.0.28 MSHAHARA – TGHS A

2.0.29 FUNDI SANIFU DARAJA LA II- UMEME (TECHNICIAN II-ELECTRICAL) NAFASI 15 2.0.30 MAJUKUMU YA KAZI


i.Kufanya ukaguzi wa ubora wa magari ya Serikali na kurekebisha ipasavyo; ii.Kufanya upimaji wa Mitambo na Umeme kufuatana na maelekezo ya Mhandisi;
iii.Kufanya matengenezo ya mifumo ya umeme;
iv.Kufanya kazi za kutengeneza mitambo,magari na vifaa vya umeme; na
v.Kufanya usanifu wa miradi midogo midogo ya umeme (kusimamia jinsi ya kufunga mashine mpya zinazowekwa kwenye karakana za Ufundi na Umeme.

2.0.31 SIFA ZA MWOMBAJI
i.Waliohitimu kidato cha nne (IV) na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani ya Umeme

ii.Waliohitimu kidato cha Sita (VI) na kufuzu mafunzo ya ufundi wa miaka miwili kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za Umeme.

iii.Wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Hatua ya I katika mojawapo ya fani za Umeme kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali,

iv.Wenye Stashahada ya kawaida katika mojawapo ya fani za Umeme kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

2.0.32 MSHAHARA – TGS C

2.0.33 KATIBU WA AFYA II (HEALTH ADMNISTRATOR II) – NAFASI 5 2.0.34 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutoa tafsiri ya Sheria, Miongozo, Kanuni za kudumu za utumishi na nyaraka mbalimbali za Serikali.
ii. Kutayarisha mipango na makisio ya fedha za shughuli zinazohusiana na afya.
iii. Kutayarisha taarifa za shughuli za uendeshaji na utekelezaji za Mwezi, Robo Mwaka na Mwaka Mzima.
iv. Kusimamia matumizi ya fedha na ununuzi wa vifaa kama ilivyo katika miongozo ya fedha na ununuzi.
v Kusimamia na kutathmini utendaji wa kazi wa watumishi kulingana na taratibu zilizokubalika. vi. Kuandaa mipango ya usafiri kwa wagonjwa.
vii. Kutoa ushauri wa kiutawala katika masuala ya kila siku kuhusu utekelezaji wa shughuli za afya. viii. Kuhifadhi takwimu na kumbukumbu za afya.
ix. Kufundisha watumishi utunzaji wa rasilimali za afya ( watumishi, fedha, vifaa na muda).
x. Kufanya utafiti.
xi. Kusimamia na kutathmini uendeshaji shughuli za afya.
xii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

2.0.35 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Uongozi wa Huduma za Afya (Health Service Administration) kutoka vyuo vinavyo tambulika na Serikali.

2.0.36 MSHAHARA – TGS D

2.0.37 AFISA TEHEMA II- FANI YA USALAMA WA MIFUMO YA TEHAMA II (ICT SECURITY) NAFASI 2 2.0.38 MAJUKUMU YA KAZI
i.Kusimamia maboresho ya programu za kompyuta kwa wakati.
ii.Kusakinisha, kusanidi na kuboresha programu za kuzuia virusi vya Kompyuta.
iii.Kuelimisha hatari na watumiaji masuala mbalimbali yanayohusu udhaifu katika mifumo ya TEHAMA. iv.Kukagua mifumo ya TEHAMA mara kwa mara.
v.Kuweka viwango vya usalama na udhibiti katika mifumo ya TEHAMA kwa watumiaji.
vi.Kufanya kazi nyingine atakazo pangiwa na mkubwa wake wa kazi zinazoendana na" sifa na fani yake.
2.0.39 SIFA ZA MWOMBAJI
Mhitimu wa Stashahada ya juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Uhandisi wa Kompyuta, Sayansi ya Kompyuta,Teknolojia ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano au Menejimenti ya Mifumo ya Habari.
2.0.40 MSHAHARA – TGS E




2.0.41 AFISA TEHEMA II –FANI YA USIMAMIZI WA MITANDAO YA TEHAMA( ICTNETWORK) NAFASI 2

2.0.42 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusanifu, kusakinisha na kusanidi miundombinu ya ndani na nje ya mtandao wa Kompyuta ii. Kufanya majaribio ya vifaa vya mtandao wa Kompyuta
iii.Kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya usalama wa mtandao kwa mujibu wa miongozo ya usalama wa mtandao wa kompyuta iv.Kutathmini na kurekebisha hitilafu zozote za mtandao wa Kompyuta
v.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkubwa wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.
2.0.43 SIFA ZA MWOMBAJI
Mhitimu wa Stashahada ya juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Uhandisi wa Kompyuta, Sayansi ya Kompyuta, Elektroniki na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.
2.0.44 MSHAHARA – TGS E

2.0.45 AFISA TEHEMA II- FANI YA UCHAMBUZI WA MIFUMO YA KOMPYUTA (ICT –COMPUTER SYSTEM ANALYST) NAFASI 2

2.0.46 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuweka kumbukumbu na taratibu za kisasa na mbinu za kufanyia kazi. ii. Kutekeleza chati za mtiririko wa mifumo ya nyendo za taarifa na udhibiti, iii. Kuandika programu za Kompyuta
iv.Kufanya majaribio ya sehemu timilifu za programu za Kompyuta v.Kufanya majaribio ya usanidi wa mifumo ya TEHAMA
vi.Kufanya majaribio ya progamu za kompyuta kulingana na mahitaji ya watumiaji vii.Kufanya kazi nyingine atakazo pangiwa na mkubwa wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake
2.0.47 SIFA ZA MWOMBAJI
Muhitimu wa Stashahada ya juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Sayansi ya Kompyuta au Menejimenti ya Mifumo ya Habari.
2.0.48 MSHAHARA – TGS E

2.0.49 AFISA TEHEMA II (MOBILE APPLICATION) NAFASI 2 2.0.50 MAJUKUMU YA KAZI
2.0.51 i. Kuandaa, kuandika na kufanya majaribio ya programu (Plan, code and test program), Kusahihisha programu (Debug program); ii. Kuweka na kuhakikisha usalama wa programu (Incorporate security setting into program); iii. Kushirikiana na wadau wengine katika kutengeneza programu mbalimbali (Corporate with other software developers); na iv.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkubwa wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.
2.0.52 SIFA ZA MWOMBAJI
Muhitimu wa Stashahada ya juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Uhandisi wa Kompyuta, Sayansi ya Kompyuta, Elektroniki na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.

2.0.53 MSHAHARA – TGS E

2.0.54 AFISA TEHEMA II (DATA ANALSTY) NAFASI 2

2.0.55 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutambua vyanzo muhimu vya data na kubinafsisha michakato ya ukusanyaji
ii. Kufanya usindikaji wa awali wa data iliyopangwa, iliyopangwa nusu na isiyo na muundo:
iii. Kuratibu uundaji, ujenzi na uwekaji wa suluhisho za akili za biashara (BI)
(k.m. zana za kuripoti) na zana za kuhifadhi data (k.m. kota za OLAP) iv. Kuchambua idadi kubwa ya habari ili kugundua mitindo na muundo v. Kuwasilisha taarifa kwa kutumia mbinu za taswira ya data vi. Kuanzisha suluhisho na mikakati ya changamoto za biashara;
vii. Kufanya tafsiri ya Data na kutoa ripoti muhimu
viii. Kutathmini ufanisi, ubora na usahihi wa vyanzo vipya vya data na mbinu za kukusanya data
ix. Kutengeneza zana za kufuatilia na kuchambua utendaji wa mfumo na usahihi wa data;
x. Kufuatilia utendaji dhidi ya malengo ya vipimo mbalimbali vya mfumo na biashara



2.0.56 SIFA ZA MWOMBAJI
Mhitimu wa Stashahada ya juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Uhandisi wa Kompyuta, Sayansi ya Kompyuta, Elektroniki na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.

2.0.57 MSHAHARA – TGS E 2.0.58 AFISA TEHEMA II (SYSTEM ADMINISTRATOR) NAFASI 2 2.0.59 MAJUKUMU YA KAZI
i.Kuchambua na kukusanya mahitaji ya watumiaji wa programu ya Kompyuta, ii. Kufanya majaribio ya sehernu timilifu za programu za Kompyuta iii. Kufanya majaribio ya usanidi wa mifumo ya TEHAMA
iv. Kufanya majaribio ya program za Kompyuta kulingana na mahitaji ya watumiaji
v. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkubwa wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.
2.0.60 SIFA ZA MWOMBAJI
Mhitimu wa Stashahada ya juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Uhandisi wa Kompyuta, Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano au Menejimenti ya Mifumo ya Habari.
2.0.61 MSHAHARA – TGS E

2.0.62 MPIMA ARDHI DARAJA LA II (LAND SURVEYOR II) DARAJA LA II – NAFASI 4

2.0.63 MAJUKUMU YA KAZI

i.Kuingiza taarifa za Upimaji (alpha numeric data) kwenye kompyuta.
ii. Kukagua kazi za upimaji na kuingiza taarifa za kazi zilizothibitishwa kwenye komputa.
iii.Kufanya upimaji picha (aerial triangulation and block adjustment); iv.Kusimamia na kuchukua vipimo vya tide gauges v. Mpima Ardhi katika Serikali za Mitaa
2.0.64 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada ya juu/Shahada kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi katika fani ya Upimaji Ardhi au Taasisi yoyote inayotambuliwa na National Council of Professional Surveyors (NCPS).
2.0.65 MSHAHARA – TGS E

2.0.66 AFISA ARDHI MSAIDIZI II (ASSISTANT LAND OFFICER II) - NAFASI 20 2.0.67 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuingiza kumbukumbu katika kompyuta; ii. Kutoa ushauri kwa wateja; iii. Kupokea, kukagua na kusambaza majalada kwa maafisa kwa utekelezaji.
iv. Kusaidia Maafisa Ardhi katika ukaguzi na kuchukua kumbukumbu, picha taarifa, vipimo vya majumba na michoro;
v. Kujumuisha na kuandaa taarifa za ukaguzi; vi. Kuandaa rasimu za Hati na uingizaji wa plani ya Hati (deed plan); vii. Kuagiza plani za Hati (Deed Plan).
2.0.68 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI), waliofuzu mafunzo ya miaka miwili ya Umiliki Ardhi na Uthamini kutoka Vyuo vya Ardhi au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
2.0.69 MSHAHARA – TGS C
2.0.70 FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UJENZI)-TECHNICIAN II (CIVIL) NAFASI 20 2.0.71 MAJUKUMU YA KAZI
i.Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga mabomba; ii.Kuchonga vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”;
iii.Kufanya kazi za upimaji (survey) wa barabara, majengo na mifereji kama atakavyoelekezwa;
iv.Kuwapangia kazi Mafundi sanifu wasaidizi na kuhakikisha wanamaliza kama ilivyopangwa.
2.0.72 SIFA ZA MWOMBAJI
i.Waliohitimu kidato cha Sita (VI) na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani za fundi ujenzi; ii.Waliohitimu kidato cha Nne (IV) na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika fani za fundi ujenzi; iii.Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I ( ujenzi) kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali; iv.Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za fundi ujenzi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
2.0.73 MSHAHARA – TGS C

2.0.74 MSAIDIZI WA HESABU II (ACCOUNTS ASSISTANT II)- NAFASI 50

2.0.75 MAJUKUMU YA KAZI

i.Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu; ii.Kutunza kumbukumbu za hesabu; iii.Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki; na iv.Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

2.0.76 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali au Cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.
2.0.77 MSHAHARA – TGS B

2.0.78 AFISA HESABU MSAIDIZI II (ASSISTANT ACCOUNTS OFFICER II) –

NAFASI 10

2.0.79 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu;
ii. Kutunza kumbukumbu za hesabu;
iii. Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki; na
iv. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
2.0.80 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti cha stashahada ya Uhasibu (Diploma) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
2.0.81 MSHAHARA – TGS C

2.0.82 AFISA MIFUGO MSAIDIZI DARAJA LA III- (LIVESTOCK FIELD OFFICER III)NAFASI 20

2.0.83 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kutoa huduma za ugani katika uendelezaji wa mifugo na mazao yake;
ii. Kutibu mifugo na kutoa taarifa za magonjwa, tiba na chakula;
iii. Kusimamia utendaji kazi wa Wahudumu Mifugo;
iv. Kutunza takwimu na taarifa mbalimbali za mifugo;
v. Kukagua ubora wa mazao ya mifugo;
vi. Kusimamia ustawi wa wanyama; na
vii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi zinazohusiana na fani yake.

2.0.84 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato chaNne (IV) au Sita (VI) ambao wamepata mafunzo ya mifugo na kutunukiwa Astashahada ya Afya ya Mifugo na Uzalishaji (NTA Level 5) kutoka Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (Livestock Training Agency - LITA) au kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
2.0.85 MSHAHARA – TGS B


2.0.86 AFISA USAFIRISHAJI DARAJA LA II (TRANSPORT OFFICER II)– NAFASI 3 2.0.87 MAJUKUMU YA KAZI

i. .Kutayarisha gharama za uendeshaji wa usafiri kwa ajili ya kusaidia kutoa maamuzi;
ii. Kuhakikisha kuwa takwimu na kumbukumbu zinazohusu vyombo vya usafiri pamoja na mitandao yake zinatunzwa vyema na kwa usahhi;
iii. Kuandaa takwimu zinazohusu maendeleo ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji, na kuwsilisha kwa watumiaji ndani na nje ya nchi;
iv. Kukusanya takwimu za usafirishaji nchini;
v. Kukadiria na kushauri juu ya utendaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya usafirishaji; na
vi. Kutekeleza majukumu mengine yahusuyo sekta ya usafirishaji.

2.0.88 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya juu ya Usafirishaji kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.0.89 MSHAHARA – TGS D

2.0.90 MHANDISI MAZINGIRA DARAJA LA II (ENVIROMENTAL ENGINEER II)- NAFASI 5


2.0.91 MAJUKUMU YA KAZI

i.Kutoa ushauri wa namna ya kulinda mazingira kutokana na shughuli za Binadamu kama Kilimo, uvuvi, ufugaji nk

ii. Kufanya Tathimini ya Mazingira (Environmental Impact Assesment) kwa miradi inayoanzishwa hasa ya Umwagiliaji na Uwekezaji katika Kilimo.

iii. Kutoa ushauri wa namna ya kupunguza uharibifu wa Udongo utokanao na kemikali za madawa ya Kilimo, Pembejeo za Kilimo au Kemikali zingine za Viwandani zihusianazo na kilimo.

iiii. Kubuni vifaa na mikakati ya kuhakikisha kuwa maji taka na uchafu utokanao na kemikali zitokazo na Kilimo haziathiri Mazingira.

iv. Kubuni mikakati itakayohakikisha kuwa Binadamu anaishi katika mazingira yenye Afya na Rafiki kimazingira.
2.0.92 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Stashahada ya juu au Shahada ya Uhandisi Mazingira kutoka Vyuo Vikuu au Taasisi nyingine zinazotambuliwa na Serikali. Wawe na ujuzi wa kutumia compyuta.

2.0.93 MHANDISI WA UMEME DARAJA LA II (ELECTRICAL ENGINEER II) NAFASI -1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi kama “Professioinal Engineer” ili kupata uzoefu unotakiwa kufanya kazi kwa vitendo katika fani zinazomhusu ili kumwezesha Mhandisi kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.

ii. Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu ubora na bei za Mitambo na vifaa vya umeme ndani na nje ya nchi.

iii. Kupitia mapendekezo ya Miradi (Project proposals) mbalimbali ya Ufundi na Umeme yanayowasilishwa; na

iv. Kutekeleza majukumu mengine ya kiofisi atakayopangiwa na Msimamizi wake wa Kazi.

2.0.94 SIFA ZA MWOMBAJI
2.0.95 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita wenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Umeme (Electrical Engineering) kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na waliosajiliwa na Bodi za Usajili ya fani husika.

2.0.96 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E

2.0.97 AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING OFFICER II) NAFASI - 3
2.0.98 MAJUKUMU YA KAZI.
i. Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.

ii. Kutangaza Sera na Sheria za ufungaji nyuki.

iii. Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.

iv. Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki.

v. Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.

2.0.99 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

2.0.100 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.

2.0.101 AFISA UFUGAJI NYUKI MSAIDIZI DARAJA LA II (BEEKEEPING ASSISTANT II) NAFASI -1 2.0.102 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusimamia manzuki;

ii. Kutunza hifadhi za nyuki,

iii. Kukusanya takwimu za ufugaji nyuki,

iv. Kutunza kumbukumbu za kazi za utafiti,

v. Kuondoa nyuki wanaodhuru binadamu na mifugo,

vi. Kutoa leseni za biashara za mazao ya nyuki,

vii. Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wananchi juu ya ufugaji endelevu wa nyuki na matumizi bora ya mazao ya nyuki,

viii. Kutunza makundi ya nyuki wanaouma na wasiouma.


2.0.103 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya Ufugaji Nyuki kutoka Vyuo vinavotambuliwa na Serikali.

2.0.104 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

2.0.105 AFISA BIASHARA MSAIDIZI (ASSISTANT TRADE OFFICER II) NAFASI - 1 2.0.106 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa takwimu za mahitaji kutokana na bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

ii. Kuandaa takwimu zinazoonyesha tofauti kati ya mahitaji na uzalilishaji.

iii. Kuusanya na kuunganisha (Compile) nyaraka za era za Biashara na sheria za Biashara

iv. Kuandaa sifa ya Biashara na huduma ambazo zinauzwa nchi za nje kwa kila Sekta kama vile kilimo,madini, nguo na kadhalika na kuandaa sifa za kampuni zinazouza nje.

v. Kukusanya takwimu za biashara kutoka kila Wilaya, kuzichambua na kutathmini mwenendo wa biashara kwa kila Wilaya.

vi. Kukusanya takwimu kutoka kwa wafanya biashara ambao wanauza na kununua kutoka masoko ya nje kama vile SADC, EAC., EU, U.S.A.

2.0.107 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya Biashara kutoka Vyuo vinavotambuliwa na Serikali.
2.0.108 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.

2.0.109 AFISA MISITU MSAIDIZI DARAJA II (FOREST ASSISTANT OFFICER II) NAFASI -10 2.0.110 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kukusanya mbegu.

ii. Kuhudumia na kutunza bustani za miti.

iii. Kutunza na kuhudumia miti na misitu.

iv. Kufanya doria.

2.0.111 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada (Diploma) ya Misitu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

2.0.112 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.
·

2.0.113 AFISA ARDHI MSAIDIZI II (ASSISTANT LAND OFFICER II) NAFASI – 2 2.0.114 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kuingiza kumbukumbu katika kompyuta;
ii. Kutoa ushauri kwa wateja; iii. Kupokea, kukagua na kusambaza majalada kwa maafisa kwa utekelezaji.
iv. Kusaidia Maafisa Ardhi katika ukaguzi na kuchukua kumbukumbu, picha taarifa, vipimo vya majumba na michoro;
v. Kujumuisha na kuandaa taarifa za ukaguzi; vi. Kuandaa rasimu za Hati na uingizaji wa plani ya Hati (deed plan); vii. Kuagiza plani za Hati (Deed Plan).

2.0.115 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au cha Sita, waliofuzu mafunzo ya miaka miwili ya Umiliki Ardhi na Uthamini kutoka Vyuo vya Ardhi au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
2.0.116 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.

2.0.117 AFISA USHIRIKA DARAJA LA II (COOPERATIVE OFFICER GRADE II) NAFASI – 10 2.0.118 MAJUKUMU YA KAZI
Kukagua vyama vya Ushirika vya Msingi vinavyoendesha miradi ya pamoja (Jointy
Venture );
ii. Kuhamasisha uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi; iii. Kukusanya na kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa; iv. Kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi;
v. Kuratibu/kushiriki katika Elimu ya Ushirika Shirikishi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi.

2.0.119 SIFA ZA MWOMBAJI

• Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika fani ya Ushirika kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.
2.0.120 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.

2.0.121 OPARETA WA COMPYUTA MSAIDIZI II (ASSISTANT COMPUTER OPERATOR) NAFASI - 1 2.0.122 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutunza kumbukumbu za shughuli za kila siku; ii. Kugundua na kusahihisha makosa yanayotokea katika data; iii. Kufanya kazi za Kompyuta; iv. Kuchapa orodha ya makossa;
v. Kufanya programu ya matumizi; vi. Kuchapa taarifa za mwisho; na vii. Kufanya kazi chini ya usimamizi wa Opereta wa Kompyuta Daraja la II.
2.0.123 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiliwa waliomaliza kidato cha nne (IV) wenye Astashahada ya mwaka mmoja ya masomo ya awali ya Kompyuta yanayojumuisha Uendeshaji wa Kompyuta wa Msingi (Basic computer operations), Progam Endeshi (Operating system), na Program Tumizi (Application Programs) au Fundi Sanifu wa Kompyuta kutoka Kwenye Taasisi/Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.0.124 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.
2.0.125 OPARETA WA KOMPYUTA II (COMPUTER OPERATOR II) NAFASI - 1 2.0.126 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya kazi za kompyuta/programu zenye mifumo migumu kwa usimamizi wa wastani wa Maopereta wa Kompyuta Waandamizi; ii. Kurekebisha mpango wa kazi katika chumba cha kompyuta; iii. Kutunza vitabu vya matumizi ya kila siku ya kompyuta; iv. Kuhifadhi data zote zinazoingizwa katika kompyuta; na v. Kuchapa taarifa za mwisho.
2.0.127 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye stashahada ya masomo ya kompyuta kutoka kwenye Taasisi/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
2.0.128 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.

2.0.129 MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II (COMMUNITY DEVELOPMENT ASSISTANT II) NAFASI - 1 2.0.130 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusaidia kubuni na kupanga mipango na miradi ya maendeleo katika eneo lake
ii. Kusaidia uwezeshaji na upatikanaji wa mafunzo kuhusu masuala ya maendeleo katika eneo lake
iii. Kushiriki katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
iv. Kusaidia kutoa elimu kuhusu kazi za kujitegemea katika eneo lake,
v. Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya jamii kila mwezi kwa uongozi wa kijiji na kwa Msimamizi wake wa kazi,
vi. Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo. vii. Kutambua na kuwezesha kaya masikini kuinua uchumi wao kupitia fursa na rasilimali zinazowazunguka.
viii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.


2.0.131 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa waliomaliza kidato cha nne (IV) wenye Astashahada (Certificate) ya Maendeleo ya Jamii kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo wa fani zifuatazo:- Maendeleo ya Jamii (Community Development), - Sayansi ya Jamii (Sociology), - Masomo ya Maendeleo (Development Studies), - Mipango na Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management), - Jinsia na Maendeleo (Gender and Development), - Rural Development, Au fani nyingine zinazofanana na Maendeleo ya Jamii.
2.0.132 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.
2.0.133 MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO ENGINEER)- NAFASI 2 2.0.134 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo; ii. Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana; iii. Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji; iv. Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji;
v. Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji;
vi. Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji;
vii. Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji;
viii. Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo; ix. Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta;
x. Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora na xi. Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji ipasavyo.

2.0.135 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji au cha Zana za Kilimo kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
2.0.136 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E.

2.0.137 FUNDI SANIFU DARAJA LA II UPIMAJI ARDHI (LAND TECHNICIAN SURVEY II) NAFASI – 20 2.0.138 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupanga na kuandaa mahitaji ya kambi za upimaji vifaa vya upimajoi na mahitaji ya jumla
ii. Kufanya upimaji wa awali na kusimika ardhini alama za upimaji
iii. Kufanya upimaji na kukusanya taarifa na takwimu zote za upimaji
iv. Kuchora “Sketch” ya mchoro ya upimaji
v. Kufanya mahesabu ya upimaji

2.0.139 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani za upimaji ardhi kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

2.0.140 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

2.0.141 FUNDI SANIFU DARAJA LA II RAMANI (LAND TECHNICIAN MAPPING II) URASIMU RAMANI - CARTOGRAPHY (NAFASI – 03) 2.0.142 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya maandalizi ya uchoraji wa ramani za miji kadiri ya uwiano unaohitajika ii. Kutunza kumbukumbu za ramani na plani
iii. Kuchora plani za hati miliki, upimaji, mashamba na vijiji
iv. Kutoa nakala za plani za hati za viwanja, mashamba na vijiji

2.0.143 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani za ramani katika kada ya arasimu ramani (cartography) kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
2.0.144 FUNDI SANIFU DARAJA LA II RAMANI (LAND TECHNICIAN MAPPING II) (UPIMAJI PICHA) PHOTOGRAMMETRY - NAFASI 3 2.0.145 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kuwianisha picha za anga na ramani na kutayarisha “photo index”
ii. Kutunza kumbukumbu za picha za anga na ramani za photogrametria
iii. Kutunza kumbukumbu za uchoraji wa ramani
iv. Kuchora ramani katika uwiano mbalimbali

2.0.146 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani za ramani katika kada ya Upimaji ramani (photogrammetry) kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali

2.0.147 FUNDI SANIFU DARAJA LA II RAMANI (LAND TECHNICIAN MAPPING II) (UCHAPISHAJI WA RAMANI)PHOTOLITHOGRAPHY - NAFASI 1

i. Kuandaa vifaa vya uchapaji wa ramani, vitabu , vipeperushi n.k
ii. Kutoa nakala za pichaza anga katika uwiano mbalimbali
iii. Kufanya maandalizi yanayohusu upigaji picha wa ramani na picha za anga
iv. Kuchapa ramani.

2.0.148 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani za ramani, Uchapishaji picha (photolithography), kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

2.0.149 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

2.0.150 FUNDI SANIFU DARAJA LA II UTHAMINI (LAND TECHNICIAN VALUATION II) NAFASI – 03

2.0.151 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuchukua taarifa za awali za uthamini kama vile vipimo vya majengo,
ii. Kuhesabu mazao na samani kwa ajili ya fidia’
iii. Kupiga picha majengo na wafidiwa,
iv. Kutayarisha michoro ya majengo na kufanya mahesabu ya awali.


2.0.152 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ma ufundi ya miaka miwili katika fani za usimamizi ardhi na uthamini kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
2.0.153 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

2.0.154 FUNDI SANIFU MSAIDIZI UJENZI II (ASSISTANT TECHNICIAN CIVIL) NAFASI - 3 2.0.155 MAJUKUMU YA KAZI

i.Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba kupaka rangi na kufunga mabomba; ii.Kuchonga vifaa vya nyumba za Serikali ikiwa ni pamoja na samani; na
iii.Kupangiwa kazi nyingine kutegegemeana na ujuzi, uzoefu na uwezo wa utendaji mzuri wa kazi na Mamlaka zinazohusika katika fani husika.
2.0.156 SIFA ZA MWOMBAJI
Wahitimu wa Kidato cha Nne (IV) waliofaulu masomo ya Hisabati na Fizikia na wenye Cheti cha mafunzo ya mwaka mmoja ya fani za ufundi (Ujenzi) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
2.0.157 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.

MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba nafasi na wanapaswa kuonesha aina ya ulemavu walionao kwenye “Ajira Portal” kwa ajili ya utambuzi kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;

iii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iv. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Baraza la Elimu ya Ufundi Tanzania (NACTE).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 18 Julai, 2023.

Muhimu, kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P. 2320, CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM) JENGO LA UTUMISHI/ASHA ROSE MIGIRO, DODOMA.
i. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/
Job Info
Job Category: Accounting/ Finance jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: Friday, July 21 2023
Duty Station: Dar es Salaam
Posted: 12-07-2023
No of Jobs: 1
Start Publishing: 13-07-2023
Stop Publishing (Put date of 2030): 12-07-2024
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.